KISHE
Monday, December 24, 2012
Sunday, November 25, 2012
STARS WAANZA MAZOEZI - SAMATTA NA ULIMWENGU BADO HAWAJAFIKA KAMBINI
Kampala
Kocha wa Timu ya Tanzania Bara, Kilimanjaro Stars, Kim Poulsen amesema ana imani na timu yake itakayotupa karata ya kwanza leo (Jumapili) dhidi ya Sudan katika mashindano ya CECAFA Challenge.
Alisema suala la wachezaji Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu kutofika mpaka sasa halimtatizi kwa kuwa ameiandaa timu vizuri na atawatumia wachezaji waliopo.
“Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu wanaweza wasicheze katika mechi ya kesho kwa sababu hawajafika lakini mimi nikiwa kocha nimejiandaa vizuri na nina imani na wachezaji waliopo,” alisema.
“Nina imani TFF wanafuatilia suala hili na wachezaji hawa watajiunga na wenzao hivi karibuni lakini hii haituzuii kufanya vizuri kwani tumejiandaa vizuri,” alisema.
Kuhusu wachezaji kama Aggrey Morris, Mohamed Nassoro na Mwadini Ali kutoka Zanzibar kujiunga na wenzao kuichezea Zanzibar Heroes, Poulsen alisema pengo lao halitampa tatizo kwa kuwa ni changamoto.
“Timu hii ambayo inadhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager kwa sasa ina wachezaji wengi chipukizi kwa hivyo huu ndio muda wa kuwapima vizuri kwani kwani haya ni mashindano makubwa,” alisema.
Alisema wachezaji wote wana hali nzuri na wana ari ya kushinda mechi yao ya kwanza dhidi ya Sudan ambazi zimo katika Kundi B pamoja na Burundi na Somalia ambazo zitacheza leo pia.
Timu za kundi A zilitarajiwa kucheza jana ambazo ni Kenya dhidi ya Uganda na Ethiopia dhidi ya Sudan Kusini.
Kundi C inajumuisha Zanzibar na Eritrea na Rwanda dhidi ya Malawi.
Sunday, November 25, 2012
UGANDA YAWACHINJA KENYA KATIKA UFUNGUZI WA CHALENJI CUP
WANAFUNZI WA CHUO CHA RCT WAENDA LIKIZO
Wanafunzi wa chuo cha RCT wa ngazi ya Stashada na Astahada wamemaliza mitihani yao hii leo na kuanza rasmi likizo yao ya miezi miwili, ambapo wanataraji kufungua tarehe 29 january 2013.
Akiongea na wanafunzi hao mkuu wa taaruma chuoni hapo bwana Nsjigwa Mwalugaja amewatataka wanafunzi hao kwenda nyumbani kupumzika huku pia wakiendelea kujiandaa kwa ajili ya muhula ujao
Aidha bw. Mwalugaja amewataka wanafunzi hao kuwakumbusha wazazi pamoja na walezi wao kuwapatia karo mapema ili waweze kupokelewa chuoni.
Akiongea na wanafunzi hao mkuu wa taaruma chuoni hapo bwana Nsjigwa Mwalugaja amewatataka wanafunzi hao kwenda nyumbani kupumzika huku pia wakiendelea kujiandaa kwa ajili ya muhula ujao
Aidha bw. Mwalugaja amewataka wanafunzi hao kuwakumbusha wazazi pamoja na walezi wao kuwapatia karo mapema ili waweze kupokelewa chuoni.
Subscribe to:
Posts (Atom)

